Mtoto kaumbwa kaumbika
Meno ya maziwa kapangika
Metulia tena merithika
nimuite nani nasiwa rika
Mwendo wa kitausi
Midomo yake nyeusi
Umbo chupa ya pespsi
Mola Kamuumba harisi
Manani nijalie mie
Hu mrembo Nijipatie
Watoto anizalie
Nyimbo nimtungie
Namtazama kilala
Nywele nyeusi bila ila
Mate hunidondoka kila
Apanuapo domo la duara.
Tamati sha timia
wino tena stazidia
Ya Malkia sha washairia
Japo kwangu hajaingia.
No comments:
Post a Comment